Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Melivita za China zatinga Dar es Salaam
2014/01/06
 

Melivita za China zatinga Dar es Salaam

<Habari Leo> 2013.12.30

 

MELIVITA mbili za kijeshi za nchini China, jana zimetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni katika ziara ya siku nne ya kirafiki kuanzia jana.

Ziara hiyo inalenga kubadilishana uzoefu na Jeshi la Wanamaji la Tanzania. Tanzania imekuwa ni nchi ya kwanza kutembelewa na kikosi hicho cha wanamaji wa China.

 

Balozi wa China nchini, Dk Lu Youquing alisema kuwa lengo la kutembelewa na jeshi hilo ni kuimarisha ushirikiano baina ya majeshi ya Tanzania na China.

 

Alisema uhusiano zaidi unahitaji kujengwa kati ya nchi hizo mbili na pia nchi hizo zina uhusiano mzuri wa kidiplomasia tangu mwaka 1964 na inahitajika kujengwa na kuwa imara kuliko sasa.

 

"Tangu wakati huo, uhusiano kati ya nchi hizi mbili umekuwa ukiendelea kuwa imara na endelevu bila shaka na ushirikiano katika nyanja nyingi utazidi kuongezeka na kuwa imara," alisema.

 

Kaimu Kamanda wa Kundi hilo, Xiao Minsheng alisema kuwa shughuli zitakazofanyika katika ziara hiyo ni pamoja na kutembelea manowari hizo na kubadilishana ujuzi na pia kufanya mazoezi baharini.

 

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji nchini, Rogastian Shaaban alisema ziara hiyo itasaidia kuboresha maradufu uhusiano uliopo kati ya Tanzania na China.

 

Alisema kuwa baadhi ya mambo watakayojifunza wanajeshi wa Tanzania kutoka kwa Wachina, itakuwa ni muhimu zaidi kwani wataongeza ujuzi katika kukabiliana na uhalifu wa baharini.

 

 

Suggset To Friend:   
Print