Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Hotuba ya M.H. Balozi LU Youqing Katika Sherehe ya Miaka Hamisini ya Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya China na Tanzania na "Focus on Africa, Happy Chinese New Year in Tanzania 2014"
2014/01/28
 M.H Dkt. Mary Nagu, Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji,

M.H. Dkt. Asha Rose Migiro, Waziri wa Katiba na Sheria,

M.H Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Ardhi,

M.H. Dkt.Seif.S.Rashid, Waziri wa Afya,

M.H. Masele, Naibu Waziri wa Nishati na Madini,

M.H. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje,

M.H.Mvihava, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha,

M.H. Lt.Gen.Makakala, Mkuu wa NDC,

M.H. Mawaziri na wabunge,

M.H. Mabalozi,

Wageni walikwa,

Mabibi,Mabwana, na Wachina wenzangu,

 

      Habari ya Usiku!

      Mwaka Mpya wa Kichina inakuja hivi karibuni, katika sikuku hii, kwa niaba ya Ubaolizi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, nawatakia Wachina nchini Tanzania, marafiki wenzanggu wa Tanzania, mabalozi wote nchini Heri ya Mwaka Mpya na Kila la Heri!

      Siku ya mwaka mpya katika kalenda ya kichina pia inaitwa Sikukuu ya Spring,ambayo ni sikukuu muhimu ya kijadi nchini China, Wachina wote wanaisherehekea sana. Sikukuu ya Spring inamaanisha kwamba majira ya spring itakuja haraka, na maumbele yote yatakuwa na uhai tena. Katika sikukuu hiyo, watu wa China wanatumaini kuwa na mwanzo mpya na maisha mazuri katika mwakani, pia wanazingatia zaidi mapenzi ya familia na ya marafiki kutokana na Sikukuu ya Spring. Hivyo, tumeiletea Tanzania sherehe hiyo ya mwaka mpya wa China, na kuisherehekea Sikukuu ya Spring pamoja na marafiki wetu wa Tanzania. Jambo la kutufurahia ni kwamba, chini ya jitihada za pande zetu mbili, sherehe hiyo iitwayo "Sikukuu ya Spring yenye Furaha------Tuko Afrika na kusherehekea Mwaka Mpya wa China nchini Tanzania" imefanyika kwa miaka mitano kwa mfululizo. Pia imewatolea wachezaji wa China na wa Tanzania nafasi nzuri ili kuonyesha mbinu wao katika jukwaa hilo, na wananchi wa pande mbili wangepata fursa ya kuona utamaduni na sanaa katika nchi zetu mbili. Sherehe hiyo imekuwa maarufu sana katika sekta ya mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Tanzania, na imekuwa sifa mpya muhimu ya kuonyesha urafiki mkubwa kati ya China na Tanzania. Leo kwa kutumia nafasi hiyo nzuri, kwa niaba ya Ubalozi wa China, nataka kutoa shukrani zangu za dhati kwa uungaji mkono wa Serikali ya Tanzania pamoja na Wizara ya habari, vijana, utamaduni na  michezo ya Tanzania, pia nawashukuru sana wachezaji na wafanyakazi wote katika sherehe hiyo.

      Mabibi, Mabwana na Wachina wenzangu, "Sikukuu ya Spring yenye Furaha------Tuko Afrika na kusherehekea Mwaka Mpya wa China nchini Tanzania" wa mwaka huu ni maalumu sana. Mwaka huo ni miaka hamsini ya muungano wa Tanzania, na vilevile ni Miaka Hamisini ya Kidiplomasia Uhusiano baina ya China na Tanzania. Miaka himisi hivi, urafiki baina ya nchi hizi mbili unaendelea vizuri sana kabisa. Hasa mwezi wa tatu, mwaka jana, kwa mwaliko wa M.H. Rais Kikwete, Rais wa China Xi Jinping alifanya ziara yake nchini tanzania, na nchi hizi mbili ziliamua kujenga na kukuza uhusiano wa ushirikiano na wa kiwenzi kwa pande zote kwa njia ya kunufaishana. Na hii imeshaweka nguvu mpya katika uhusiano baina ya China na Tanzania. Mwaka ulioptia, ziara za kiwango cha juu baina ya nchi hizi mbili zilifanywa mara nyingi, na ushirikiano wa nchi hizi mbili umepata mafanikio makubwa sana.Takwimu kutoka Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania imeonyesha kwamba, China imekuwepo nafasi ya pili katika nchi za nje za uwekezaji nchini Tanzania,, China imekuwepo nafasi ya pili katika nchi za nje za uwekezaji nchini Tanzania,China imewapa Watanzania nafasi za ajira zaidi ya laki moja. Vilevile,  China imekuwa soko kuu la biashara kwa Tanzania. Idadi ya kiasi cha biashara kati ya China na Tanzania imefikia Dola Bilioni 2.47 za Merikani, Watanzania zaidi ya laki 3.5 wanafanya kazi kuhusu biashara na China. Kwa msaada wa mkopo nafuu wa Dola Bilino 1.2 za Merikani, Mradi wa Bomba la Gesi la Mtwara unaendelea vizuri sana sana. Siku mbili iliyopita, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Professa Muhongo na mimi, M.H Waziri Mkuu ameshatembelea Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi huu, na tunafurahi sana kuona mafundi wa China na Tanzania wanashirikiana kwa karibu, na katika upande wa maendeleo, ubora, usalama na ulinzi wa mazingira, mradi huo unaendelea vizuri sana. Zaidi ya hayo, kwa ushirikiano wa nchi hizi mbili, Bandari ya Bagamoyo na kituo cha umeme cha Kinyerezi zinaendelea vizuri sana kabisa, miradi hii inawasaidia sana maendeleo ya uchimi ya Tanzania, na itaboresha sana kiwango watanzania wanaoishi, na vilevile, itazidishi urafiki baina ya China na Tanzania.

      Sherehe hiyo ni kama mwanzo wa shughuli husika za maadhimisho ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kwa miaka 50 kati ya China na Tanzania., serikali ya China na ya Tanzania zitaandaa sherehe za kila aina, tutawasiliana na shirikiana katika sehemu yoyote na upande wowote. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuzidisha uhusiano wa urafiki baina ya China na Tanzania.

      Mabibi Mabwana na Wachina Wenzangu,

      Sasa, watu wa China wanafanya kazi kwa bidii sana ili kutambua ndoto ya Rejuvenation ya nchi yetu, na vilevile, watu wa Tanzania na Africa wanafanya kazi kwa bidii sana ili kutambua ndoto ya maendeleo na inua za nchi zao. Katika mwaka mpya, ni lazima tuunganane mikono ili kupata maendeleo makubwa katika njia ya kuitambua ndoto zetu!

      Mwishoni, kwa moyo wa dhati, nawataika mafanikio ya China na Tanzania, furaha kubwa ya Watu wa China na Tanzania, na vilevile, urafiki baina ya China na Tanzania udumu milele!

      Asanteni Sana!

 

Suggset To Friend:   
Print