Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Wachina waahidi kulinda viwango
2014/01/28
 

Na Eliza Edward, Mwananchi
Posted  Alhamisi,Januari23  2014  saa 24:0 AM

 

Dar es Salaam. Chama cha Wafanyabiashara kutoka nchini China wanaofanya shughuli zao chini ya mwamvuli wa Kariakoo Chinese Chamber of Commerce (KCCC), kimetoa ahadi ya kulinda viwango vya ubora wa bidhaa zinazosambazwa na wanachama wake.

Pia, chama hicho kitaendelea kusimamia viwango vya ubora vilivyowekwa na mamlaka mbalimbali, ili kuboresha mazingira ya biashara eneo la Kariakoo na kulinda hadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini China.

Katika hatua ya awali ya kutekeleza hilo, chama hicho jana kilishirikisha wanachama wake kusaini mapendekezo maalumu ya kuboresha mazingira ya biashara zao ikiwa ni mkakati wa kukiwezesha kuzingatia ubora wa bidhaa wanazosambaza.

Akizungumza baada ya hafla hiyo Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Tu Qiang alisema wataendelea kuunga mkono shughuli mbalimbali za kukuza 'Jiji la Biashara Kariakoo' ikiwa ni jitihada zao kuunga mkono maendeleo ya uchumi nchini.

Tu alisema chama chake kitaendelea kufanyakazi na wadau wote, kutengeneza mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyabiashara kutoka China na wafanyabiashara wazawa. "Bila kupinga Kariakoo ni moja ya kituo kikubwa cha biashara Tanzania na Afrika Mashariki, wafanyabiashara wengi wa Kichina wanajipatia riziki," alisema Tu.

 

Suggset To Friend:   
Print