Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Mipango miji ni mali ya miji
2015/04/29

Mipango miji ni kitambulisho cha mji, ili kuwa na mji ni lazima kuwa na mipango miji kwanza. Rais XI Jinping aliwahi kusema kwamba, kuanzisha mji mmoja ni lazima kuandaa mipango ya mji huo, mipango ya kisayansi ina faida kubwa sana, ukosefu wa mipango miji ni kosa kubwa sana katika maendeleo ya mipango miji. Katika miaka ishirini (20) iliyopita China imepata maendeleo makubwa sana na ya haraka, tunashukuru serikari za mitaa kwani ziliona umuhimu wa kuwa na mipango miji, hivyo ilifanikiwa kupanga mji kwa usanifu wa hali ya juu. Yafwatayo ni maoni yangu katika kukuza maendeleo ya Afrika

1,Kuwa na mipango madhubuti ya ujenzi wa miundombinu ya manispaa, ulinzi wa mazingira ya asili, kuboresha mazingira ya kuishi, mazingira bora, hufanya mji ukue kwa urahisi na kwa ufanisi, na hivyo kuzidisha thamani ya ardhi, na kuvutia wawekezaji zaidi wa kigeni.

2,Kuundwa kwa miundo ya maendeleo ya mji na viwanda kwa mipango madhubuti, kama vile, kujenga eneo la viwanda(Industrial Zone), na eneo la biashara(Business Zone),ili kuepusha athari za mipango miji

3, Wakati Afrika inatarajia kuingia katika soko la dunia, uwekezaji ni wa kila aina. Ni lazima kutimiza ndoto za serikali za kuboresha ardhi na kuzuia athari zake, ili kutimiza usawa.

Zaidi ya hayo, serikali ya China huthamini usimamizi na utekelezaji, lakini pia inaona umuhimu mkubwa wa kujenga mfumo kamili wa utekelezaji, Kama vile, kila mji hufuata mfumo wa “mambo matatu” kukaguliwa, na kukubali, ili kutimiza utekelezaji wa ufanisi wa mipango ya mji.

Mambo hayo matatu ni haya yafuatavyo: kutokana na vipindi tofauti vya mradi, ni lazima kupata vibali vitatu kutoka idara husika, yaani kibali cha kuchagua eneo(site submission),kibali cha mipango ya ardhi(land planning permit), na kibali cha mipango ya kujenga mradi(construction project planning permit). Mwisho

Afrika ni bara lenye sifa za mila na utamaduni na hata kijiografia, kutoka katika mipango madhubuti ya usanifu wa majengo mazuri , yaonekanayo yamepabwa kwa tamaduni nzuri za kiafrika hivyo kuhifadhi urithi wa utamaduni, na kuvutia macho ya dunia.

 

DR.LU YOUQING, BALOZI WA CHINA

Suggset To Friend:   
Print