Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Afrika Njia Panda: Matokeo ya Vita Baridi yajirudia katikati ya Mkakati mpya wa Marekani kuhusu Afrika
2018/12/31

Francis Semwaza

Uzinduzi wa Mkakati wa Marekani kuhusu Afrika unaashiria mwelekeo mpya kabisa katika siasa za kimkakati za kijiografia hivi sasa ambapo hisia hasi za nchi za magharibi za kupambana na China zikizidi kudhihirika, hususan bara la Afrika linapohusishwa.

Imegunduliwa na mmoja wa nguli wa sera ya mambo ya nje Mshauri wa Usalama wa Taifa, Bw.John Bolton kuwa dondoo muhimu za mkakati huo ni kuanzisha vita na washindani wa kigeni huku mahitaji ya bara la Afrika na watu wake, yakisahauliwa kwa kiasi kikubwa wameachwa.

Baada ya kutaja China angalau mara 15 na nchi moja ya Kiafrika ambayo ni Sudan Kusini, ambayo ndiyo iliyotajwa zaidi, mara 5 tu, katika hotuba ya uzinduzi aliyoitoa Bolton, itafanya mtu yeyote ashangae kama kile kinachoitwa 'Mkakati wa Afrika' ni kweli unalenga Afrika kama mnufaishwa au bara hilo kama uwanja wa vita tu kukabiliana na China na Urusi!

Mbali na kuzilazimisha nchi kuchagua upande mmoja dhidi ya mwingine, na kukosoa mbinu zinazotumiwa na China barani Afrika kuwa zimegubikwa na rushwa, uamuzi wa Marekani kutumia fikra za enzi za kale katika mkakati wake barani humo umewaacha na maswali hata baadhi ya wasomi wake kwani umeshindwa kueleza namna ambavyo ungeweza kutekelezwa. Katika masikio ya wengi, inaweza kuonekana kama aina fulani ya ukoloni mamboleo unaotumia mbinu ya 'kuwagawa na kuwatawala' kuliko mpango halisi wa maendeleo.

Kutokana na uzoefu, hiki ndicho kilichotokea wakati wa kipindi cha vita baridi pale nchi kama Angola, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo nchini Afrika zilitokwa dam nyingi kugharamia michezo ya siasa za kuunga mkono vita vya kiitikadi kati ya 'magharibi' na ‘mashariki', hadithi maarufu ya mapambano kati ya ubepari na ujamaa.

Nchi za magharibi kuanzisha upya mapambano dhidi ya China na Urusi kuanza kujipanua barani humo unaliweka bara la Afrika katika njia panda ya kuweza kujitegemea ili kuhakikisha uhuru, amani na utulivu wake vinadumu kudumu: hii ikiwa ni pamoja na kuweza kujikinga dhidi ya propaganda nyepesi za kupinga maendeleo kama zile habari potofu kuwa China imeipoka kampuni ya umeme ya kitaifa ya Zambia, ZESCO, na ile ya kupokonywa kwa bandari ya Mombasa ya Kenya na China, ambazo zote si za kweli hata kidogo.

Maendeleo haya mapya lakini yaliyopitwa na wakati ya Sera ya Marekani kwa Afrika pia yamekosolewa na baadhi ya watu mashuhuri ikiwemo Mwenyekiti wa sasa wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Mheshimiwa Moussa Faki Mahamat, kama ‘kuidumaza Afrika', akihimiza kuwa Afrika iko huru kuchagua na kushirikiana na nchi yoyote kama marafiki zake.

Kujinasua katika mtego huo inaweza kuwa kazi ya ngumu kidogo kwa Afrika ikizingatiwa kufungamana na ukaribu ambao nchi mbalimbali za Kiafrika, na nchi nyinginezo zinazoendelea zimeufanya na nchi zilizoendelea: kiasi kwamba si ajabu kukuta nchi kama China, Canada, Urusi na Marekani zote kwa pamoja zikishiriki katika kuendeleza jeshi la nchi moja ya Afrika kwa mfano.

Kwa kupitia kivuli cha misaada, mataifa makubwa kadhaa ya kigeni yameweza kujipenyeza hadi kwenye kiini cha jamii mbalimbali za Kiafrika, ama ukipenda unaweza kukiita kiini hicho serikali, na hata kuweza kushawishi masuala ya msingi kadiri wanavyoona inafaa kiasi kwamba wameweza kuifahamu zaidi Afrika kuliko ambavyo Waafrika wenyewe wanaifahamu.

Ni dhahiri kuwa nchi hizo zitakuwa zikitoa misada huku zikiwa na nia mbalimbali zinazodumisha maslahi yao, jaribio ambalo China imeweza kulivuka hususan kwa kuzingatia ukweli kwamba imejikita katika kutoa misaada ya dhati kwa karne kadhaa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya msingi kama vile barabara, reli na kuendeleza bandari katika nchi kadhaa za Afrika tangu miaka ya 1960 hadi leo.

Kwa kuzingatia urefu wa muda na kiwango cha msaada ambacho kila nchi ya kigeni inaweza kuwa imetoa katika sekta fulani, kusitisha mahusiano kabisa ni jambo lisilowezekana na hivyo kufanya utekelezaji wa Mkakati wa Marekani kuhusu ya Afrika kuwa mgumui, hususan pale linapokuja suala la kupewa maelekezo ya kuchagua kati ya nchi za Magharibi kwa upande mmoja na China na Russia kwa upande mwingine.

Hali hiyo inakua ngumu zaidi kutokana na kjipenyeza hadi katika masuala ya ndani kabisa ya nchi za Afrika kulikofanywa na mataifa ya kigeni, na hivyo kufanya ndoto za Waasisi wa Mataifa yetu, ikiwemo kujitegemea, kuwa vigumu kutimizwa kwani haziwezi kuwa ajenda kama ilivyokuwa katika miaka michache baada ya kujipatia Uhuru.

Pengine ingekuwa hekima kwa nchi yoyote ya Kiafrika inayohisi kunasa katika utegemezi wa aina hii kurejea katika kufuata hekima ya zamani iliyotolewa na Kwame Nkrumah ikisema kutokwenda mashariki wala magharibi na badala yake kwenda mbele katika kuboresha ustawi wa watu wa Afrika kupitia ushirikiano, misaada na sera za kirafiki ambazo zinalenga kuiendeleza Afrika, badala ya zile zinazotaka kutibua urafiki uliopo kati ya Afrika na marafiki zake wa kuaminika, ikiwemo China.

Ingawa mwanzoni majadiliano yanaweza kuifanya hali ya mchuano kati ya nchi za Magharibi dhidi ya China na Urusi ifanane na ilivyokuwa wakati wa vita ya baridi,uhalisia unaweza kuwa mgumu zaidi kuliko inavyofikiriwa kwa sababu maslahi si ya pande moja tena, bali yanaingiliana.

Mbinu inayotumika na China barani Afrika ni ya kibiashara zaidi ambapo inalenga kugusa maisha ya Waafrika wengi wa kawaida kwa kutoa teknolojia na bidhaa za bei nafuu. Kinyume chake, mkakati mpya wa Marekani kuhusu Afrika si lazima uwe na sura ya kibiashara na matokeo yake si lazima vilevile uguse moja kwa moja mahitaji ya msingi ya watu wa Afrika kwa namna iliyo chanya.

Hata hivyo, mahusiano kati ya Marekani na China na Marekani na Urusi hayawezi kuzorota kiasi cha kufikia kuzuka vita baina yao. Mbali na umbali wa kijiografia na uwezo wa kijeshi ambao kila moja ya nchi hizo inajivunia, bado nchi hio zinahusiana kiuchumi na hutegemeana kwa namna nyingi.

Licha ya changamoto mbalimbali za hivi karibuni, China inafanya biashara zaidi na Marekani kuliko nchi nyingine yoyote; uhusiano kati ya nchi ya Urusi na Marekani, au angalau uhusiano kati ya Vladimir Putin na matajiri wengine wa Kirusi na Rais Donald Trump umekuwa mzuri, mara nyingine hata kwa gharama ya manufaa ya raia wa kawaida wa Marekani.

Utangamano huu unafanya kuwa vigumu kwa Marekani, China au Russia kupiga vita kati yao, licha ya kudhihirisha dalili za mchuano zinazofanana na siasa zilizokuweko kabla ya kufanyika ukoloni barani Afrika ambapo wakati huo Ujerumani na Italia walikuwa mataifa yenye nguvu yanayoibukia na yakaja kuchuana na mataifa makubwa yaliyotawala dunia ya Uingereza na Ufarasa.

Kinyume na nadharia ya Mtego wa Thucydides ambayo inatabiri kuvaana ana kwa ana kati ya dola zinazoibukia na zile zilizopo mlinganyo wa nguvu, umbali wa kijiografia na mahusiano ya biashara yaliyopo kati ya Marekani, China na Urusi, kwa namna moja au nyingine, vinaondoa uwezekano wa mapambano ya kivita kutotokea kati yao kwasababu kutakuwa na mengi ya kupoteza kuliko kupata. Muhimu zaidi, kukosa udhibiti kamili kati ya nchi yoyote kati ya hizo barani Afrika, na kiwango cha juu cha kujitambua barani humor, ambapo ndiyo panasemekana pangekuwa uwanja wa mapambano baina ya mataifa hayo makuba, kunafanya vigumu kanzisha vita vya kutumia wafuasi barani humor licha ya kuwepo kwa migogoro ya ndani kwenye baadhi ya nchi.

Katikati ya sintofahamu hiyo, Afrika inapaswa kujifunza kuainisha vipaumbele vyake katika kushirikiana na nchi za kigeni na kufanya maamuzi ya mwelekeo na aina ya mahusian kati yake na nchi yoyote bila kulazimishwa kudumbukia kwenye mtgo wa propaganda nyepesi za kuipinga China ambazo zinachukulia siasa za kimataifa kwa mtizamo wa kupata au kukosa - kuchagua moja, ama nchi za magharibi kwa upande mmoja au China/Urusi kwa upande mwingine.

Kutokana na kusosekana kwa mkakati wa utekelezaji wa wazi wa Mkakati wa Marekani kuhusu Afrika, Afrika haina budi kufanya ushawishi ili kunufaisha watu wake ili isitokee hali kupata au kukosa, bali wote kupata kabla hali ya sasa haijawa mbaya zaidi.

Suggset To Friend:   
Print